Umlabalaba tournament rules in Kiswahili

Sheria za mchezo wa Umabalaba (Tafsiri ya David Isiche)

Kila mchezaji anapewa tokeni 12. Kumbuka kuwa kwa Isizulu tokeni zinafahamika kama ng’ombe, lakini kwenye aina ya isipowe iliyoko kwenye BLAC Foundation kila mchezaji anapata ng’ombe tisa, wachungaji wawili (abelusi), na kundi moja la mashujaa (ibhuto). Hata hivyo, kwa minajili ya uyakinifu, tokeni zote zinahesabiwa kama ng’ombe kwa sababu zinasongezwa na kuchukuliwa kwa namna moja.

  1. Mchezaji wa kwanza huweka tokeni zake kwenye nafasi yoyote inayostahili kwenye ubao (mf. Mahali mistari miwili inakutana).
  2. Halafu mchezaji wa pili anaweka tokeni yake kwenye nafasi zilizobaki.
  3. Hapo mchezaji wa kwanza anaweka tokeni zake kwenye nafasi yoyote kwa kusudi ya kumfungia njia mpinzani wake ili asiweze kuwa na tokeni tatu zimeandamana kwa msitari mmoja ( yaani isibhamu “msitari wa kunasa”) ama kuweza kufanya “msitari wake wa kunasa” wenye tokeni tatu (mfano wa tic tac toe).
  4. Ikiwa mmoja wa wachezaji ataweza kuunda msitari wa tokeni tatu ulio wima, mlalo au uliolala (msitari wa kuteka), yeye hutoa tokeni moja ya mpinzani wake.
  5. Mchezo unaendelea hadi mchezaji wa pili anapoweka tokeni yake kwenye ubao. Hapo awamu ya pili inaanza.
  6. Baada ya mchezaji wa pili kuweka tokeni yake ya mwisho kwenye ubao, mchezaji wa kwanza anasongeza mojawapo ya tokeni zake kwa nafasi moja kwenye mistari hadi nafasi iliyo wazi ili kumzuia mpinzani wake asitengeneze msitari wa kuteka. Kumbuka, iwapo nafasi zote 24 zimetwaliwa, mtu aliyekuwa wa kwanza anafaa kutoa moja kati ya tokeni zake na kumzawadia mpinzani wake (ilobolo). Mchezaji wa pili naye anastahili kutoa na kumzawadi mpinzani wake tokeni yake moja. Kumbuka kwamba ikiwa mchezaji hawezi kusonga kutokana na kukosa nafasi ya kusonga, mpinzani wake anasonga tena.
  7. Wakati msitari wa kuteka unatengenezwa mchezaji huteka tokeni moja ya mpinzani wake.
  8. Tofauti na aina iitwayo isisuthu, wakati mchezaji ana tokeni tatu pekee zilizobaki anaweza (kwa kukataa tamaa) kusongeza tokeni yoyote kati ya hizi kwenye nafasi yoyote iliyo wazi kwenye ubao. Wakati mchezaji anateka tokeni kumi za mpinzani mchezo unaisha na anatangazwa kama mshindi.
  9. Kumbuka kwamba inawezakana mchezo usiishe ikiwa ubao utakuwa na kizuizi na kila mchezaji asongeze na kurudia mtindo mmoja. Hapo kutakuwa na usawa kwenye mchezo. Isitoshe, wakati wachezaji wote wawili wamebaki na tokeni tatu, ikiwa hakuna tokeni itatekwa kwa songezo 30 (yaani mchezaji 1 na mchezaji 2 wote wanaposongeza mara 30) mchezo unakuwa sare.